Logo Lanfrica

Athari za Usasa kwenye Usimulizi wa Hadithi katika Jamii ya Wamasaaba Nchini Uganda

Domain:

natural language processing
Creator:
WilROCNan
Publisher:
Eas
Host:
Katika makala haya, watafiti anaeleza jinsi usimulizi wa hadithi umeathiriwa na usasa katika jamii ya Wamasaaba nchini Uganda. Anafanya hivyo kwa kulinganisha hali ilivyo sasa na jinsi ilivyokuwa kabla Wazungu hawajazuru barani Afrika. Mtafiti analinganisha miktadha ya utendaji wa hadithi na anatoa maelezo kuhusu mitindo mbalimbali ya utendaji. Anaeleza jinsi Waafrika walivyosimulia watoto wao hadithi kabla ya Wazungu kuja barani humu. Kwenye kazi hii, madhumuni ya utafiti ni: kudhihirisha athari za usasa kwenye masimulizi ya kinathari. Pili, kueleza stadi zilizokuwa zikitumiwa na Waafrika katika usimulizi wa hadithi. Mkabala wa utafiti ulikuwa wa nyanjani. Kwa kutumia mkabala huu, mtafiti alizuru nyanjani halafu akaanza kuendeleza mahojiano na wahojiwa wake. Kabla hajafanya hivyo, mtafiti alijitambulisha kwa wahojiwa wake na kuwaambia sababu za utafiti wake. Alifanya hivyo ili kuwaondolea wasiwasi. Majibu ya wahojiwa yalijumlisha data ambazo zilihitajika na mtafiti. Matokeo ya utafiti yanaonyesha kuwa usimulizi wa hadithi umefifia sana katika jamii ya Wamasaaba kutokana na usasa. Sababu ambazo zimepelekea usimulizi wa hadithi kufifia jamii hii pia zimeelezwa. Miongoni mwa sababu hizo ni: ulevi ambao hufanya watu kurejea nyumbani wakiwa wamelewa na kushindwa kusimulia watoto wao hadithi. Sababu nyingine ni wazazi kuthamini elimu ya kisasa na kuacha utamaduni wao wa kulea watoto ili baadaye wawe wake na waume wazuri. Wazazi kuhamasisha watoto wao wasome vitabu badala ya kuwasimulia hadithi. Nne, wazazi kuwa na lengo la kuelimisha watoto wao ili baadaye wapate kazi za afisi. Tano, jambo la kuwepo na utandawazi ambalo limepelekea watu kujumuika na kuiga tamaduni za kigeni. Upeo wa utafiti huu ulihusika na mabadiliko kwenye usimulizi wa hadithi na sababu ambazo zimepelekea utamaduni wa kusimulia hadithi kufifia katika jamii ya Wamasaaba nchini Uganda. Mtafiti alitumia mbinu ya bahati nasibu kuteua sampuli za wahojiwa.

Similar