Logo Lanfrica

Kufundisha Kiswahili kama Lugha ya KigeniTeaching Kiswahili as a Foreign Language

Domain:

natural language processing

Record type:

paper
Creator:
Far
Publisher:
Wal
Host:
Ikisiri Ufundishaji wa lugha ya kigeni nje ya mazingira yake ya matumizi ni sekta inayokua kwa kasi duniani. Tafiti zinaonesha kwamba ni rahisi kujifunza lugha ya kigeni kwa kushiriki moja kwa moja katika mazingira ya kiutamaduni ya jamii inayozungumza lugha hiyo kila siku. Hata hivyo, kutokana na mahitaji ya kielimu na kiuchumi, maendeleo ya teknolojia, pamoja na kuongezeka kwa mwingiliano wa kimataifa, ufundishaji wa lugha ya kigeni nje ya mazingira yake ya matumizi unaendelea kukua. Hali hii inaweza kuathiri ufundishaji wa vipengele vya kiutamaduni vinavyohusiana na lugha lengwa. Lengo la makala hii ni kubainisha vipengele vya utamaduni wa Kiswahili na namna vinavyoweza kufundishwa kwa wajifunzaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni, hususan katika mazingira ambayo lugha hiyo haitumiki katika maisha ya kila siku. Vipengele vilivyobainishwa katika makala hii ni salamu, mavazi, vyakula, sherehe na misiba, tamathali za semi, imani na dini, pamoja na sanaa na burudani.

Similar