Logo Lanfrica
  • Home
  • Atlas
  • Insights
  • Docs
  • Sign in

© 2026 Lanfrica. All rights reserved. All copyrights of the resources shown on the Lanfrica website belong to the original copyright holders, unless explicitly stated otherwise.

Maongezi Katika Riwaya Za Kiswahili

Domain:

natural language processing
Creator:
DanRicJos
Publisher:
Eas
Host:
Makala hii inaangazia dhima ya maongezi katika riwaya ya Kiswahili. Riwaya ni mojawapo wa tanzu muhimu za fasihi ya Kiswahili ambayo inaendelea kukua kwa upande wa wahusika, dhamira, maudhui, mtindo na upeo. Utanzu wa riwaya ya Kiswahili ulianza mwanzo wa karne ya ishirini wakati James Juma Mbotela alipoandika riwaya ya Uhuru wa Watumwa (1934). Ukuaji wake umeshika kasi zaidi katika mwongo wa mwisho wa karne ya ishirini na mwanzo wa karne ya ishirini na moja. Ni muhimu pia kutambua kuwa, utungaji wa riwaya umeendelea kukua sambamba na uhakiki wake. Katika karne ya ishirini na moja, riwaya ya Kiswahili imefikia utungaji wa kimajaribio (Mwamzandi, 2013:48-66 na Mohamed 2003:78-79). Katika riwaya za kimajaribio, watunzi hujumuisha nadharia, visasili pamoja na kuzungumzia masuala ya utandawazi na soko huru. Ni riwaya ambazo hukiuka miundo ya riwaya iliyozoeleka. Kwa upande wa maongezi, usemaji wa wahusika katika riwaya umekua kutoka sahili hadi changamano kutokana na masuala yanayojadiliwa katika riwaya mahususi. Ni maoni ya waandishi wa makala hii kuwa, usemaji wa wahusika unaweza kuathirika na vipindi vya kihistoria hivyo basi kuwa na mchango muhimu katika maendeleo ya riwaya. Madhumuni ya makala hii ilikuwa ni kuainisha maongezi katika riwaya za Kiswahili. Riwaya ambazo zilichanganuliwa kwa mujibu wa makala hii ni Kusadikika (1951), Mafuta (1984) na Kufa Kuzikana (2003). Riwaya hizo ziliteuliwa kuwakilisha vipindi mahususi vya ukuaji na maendeleo ya riwaya ya Kiswahili. Makala hii iliongozwa na nadharia ya Uchanganuzi wa Usemi Hakiki. Kutokana na uchanganuzi huo, makala hii imebainisha mchango wa maongezi kwa ukuaji, maendeleo na uumbufu wa utanzu wa riwaya kwa ujumla.

Visit

doi.org

Languages

KwaSwahiliSwahili, CoastalSwahili, CongoTeke-Kukuya

Licenses

http://creativecommons.org/licenses/by/4.0

Similar

Ubabedume na Dhiki za Mwanamume katika Riwaya za Kiswahili za Waandishi WanawakeUamilifu wa Ngazi ya Utambuzi katika Riwaya Teule za KiswahiliUchunguzi wa fani za lugha zilivyotumika kuibua changamoto za vijana katika riwaya teule za KiswahiliUhakiki wa Mtindo katika Riwaya ya Kiswahili: Mifano Riwaya za Kidagaa Kimemwozea na Chozi la HeriMchango wa Tanzu za Kimaigizo za Fasihi Simulizi Katika Umahuluti wa Riwaya ya Kiswahili: Uchunguzi wa Riwaya ya Kufa KuzikanaBaadhi ya Mbinu za Kifani katika Riwaya ya Kiswahili "Riwaya ya Kiu ya Mohamed Suleiman kama mfano"

Ubabedume na Dhiki za Mwanamume katika Riwaya za Kiswahili za Waandishi Wanawake

Swahili  Tafiti nyingi kuhusu ubabedume katika fasihi ya Kiswahili zimejikita katika athari zake kwa

Uamilifu wa Ngazi ya Utambuzi katika Riwaya Teule za Kiswahili

Makala haya yanachunguza ngazi ya utambuzi na uamilifu wake katika riwaya za Kiswahili zilizoteuliwa

Uchunguzi wa fani za lugha zilivyotumika kuibua changamoto za vijana katika riwaya teule za Kiswahili

Utafiti huu ulilenga kuchunguza namna mbinu mbalimbali za lugha zilivyotumika kuibua na kudhihirisha

Uhakiki wa Mtindo katika Riwaya ya Kiswahili: Mifano Riwaya za Kidagaa Kimemwozea na Chozi la Heri

Utafiti huu ulikusudia kuchanganua matumizi ya mtindo katika riwaya za Kidagaa Kimemwozea (2012) ya

Mchango wa Tanzu za Kimaigizo za Fasihi Simulizi Katika Umahuluti wa Riwaya ya Kiswahili: Uchunguzi wa Riwaya ya Kufa Kuzikana

Usomaji wa fasihi katika kipindi cha sasa unabainisha idadi kubwa ya waandishi kutoka jamii zisizo W

Baadhi ya Mbinu za Kifani katika Riwaya ya Kiswahili "Riwaya ya Kiu ya Mohamed Suleiman kama mfano"

Kazi ya fasihi ikiwemo riwaya huundwa na fani na maudhui, ambavyo kwa pamoja ndivyo hutupatia kazi i