SWAHILI
Utafiti huu ulilenga kubainisha namna maudhui ya kifo yanavyochangia ukuzaji wa maudhui mengine katika riwaya Chozi la Heri ya Assumpta K. Matei. Katika fasihi, maudhui ya kifo hayajitokezi kama maudhui yanayojitegemea pekee, bali hutumika kama nyenzo ya kuibua, kuendeleza na kuimarisha maudhui mengine yanayohusu maisha na jamii. Utafiti uliongozwa na Nadharia ya Udhanaishi kwa mujibu wa Sartre (1948) na ulitumia muundo wa kimaelezo. Data za msingi zilikusanywa kutoka Chozi la Heri, iliyoteuliwa kimakusudi, huku data za sekondari zikikusanywa maktabani kutoka vitabu, majarida na tasnifu zinazohusiana na mada. Data zilichanganuliwa kimaelezo kwa kuongozwa na mhimili teule wa Nadharia ya Udhanaishi na kuwasilishwa chini ya mada ndogo zilizotokana na maudhui yaliyobainika. Matokeo yalionyesha kuwa maudhui ya kifo yalichangia ukuzaji wa maudhui ya ukoloni mkongwe, ukoloni mamboleo, uongozi mbaya, dini, dhuluma, ukatili na mitazamo ya jamii kuhusu jinsia ya kiume. Utafiti huu unatarajiwa kuwanufaisha wanafunzi, walimu, wahakiki na wanazuoni wa fasihi ya Kiswahili kwa kupanua uelewa kuhusu namna maudhui ya kifo yanavyohusiana na kukuza maudhui mengine katika kazi za fasihi.
ENGLISH
This study aimed to examine how the theme of death contributes to the development of other themes in Assumpta K. Matei’s novel Chozi la Heri (2014). In literary works, the theme of death does not occur as an independent theme alone; rather, it serves as a device through which other themes related to human life and society are introduced, developed, and reinforced. The study was guided by Sartre’s (1948) Existentialist Theory and adopted a descriptive research design. Primary data were obtained from Chozi la Heri, who was purposively selected, while secondary data were obtained from library sources, including books, journals, and theses related to the study. The data were descriptively analysed using a selected tenet of Existentialist Theory and presented under sub-themes derived from the themes identified. The findings revealed that the theme of death contributed to the development of the themes of colonialism, neo-colonialism, bad leadership, religion, oppression, brutality, and societal perceptions of masculinity. The study is expected to benefit students, teachers, literary critics, and scholars of Kiswahili literature by broadening their understanding of how the theme of death relates to and contributes to the development of other themes in literary works.
Keywords: Death, existentialism, novel, themes