Logo Lanfrica
  • Home
  • Atlas
  • Insights
  • Docs
  • Sign in

© 2026 Lanfrica. All rights reserved. All copyrights of the resources shown on the Lanfrica website belong to the original copyright holders, unless explicitly stated otherwise.

Muundo wa Kifonolojia wa Maneno ya Sheng’

Domain:

natural language processing

Record type:

paper
Creator:
JotDav
Publisher:
Eas
Host:
Utafiti huu ulidhamiria kutathmini athari za kamusi ya Sheng’ – English Dictionary kwa Kiswahili sanifu. Kamusi ya Sheng’ – English Dictionary (2003) iliteuliwa kama msingi wa uchunguzi huu kwa sababu ndio kamusi ya kwanza ya Sheng’ kuwahi kuchapishwa. Licha ya kamusi hii kuchapishwa katika lugha ya Kiingereza ina leksimu za Sheng’ ambazo yafaa kuchunguzwa namna zinavyoathiri Kiswahili sanifu. Lengo la utafiti huu lilikuwa kueleza muundo wa kifonolojia wa maneno ya Sheng’ na jinsi yanavyotofautiana na Kiswahili sanifu. Nadharia ya utafiti ilikuwa Nadharia ya Fonolojia Boreshi ambayo inapatikana katika mtazamo mpana wa Nadharia Boreshi iliyoasisiwa na Alan Prince na Paul Smolensky (2003). Hii ni nadharia inayochunguza hatua za ukuaji wa msamiati kutoka hali ghafi hadi ukubalifu wake kupitia kwa vizuizi tofauti. Mahali pa utafiti palikuwa maktabani na mtandaoni. Mbinu ya uchunguzi ikawa kupitia kusikiliza na kusoma makala mbalimbali kuhusu mada hii. Data ilikusanywa kupitia kwa kuchunguza maneno na vidahizo vya maneno kutoka kamusi ya Sheng’ – English Dictionary (2003). Iliaminika kuwa kamusi hii ingetupa sampuli ya maneno mahsusi ya Sheng’ ambayo muundo wake huathiri matumizi katika Kiswahili sanifu kwenye jamii ya kisasa. Uchanganuzi wa maelezo ulitegemea mtazamo wa Fonolojia Boreshi katika nadharia ya fonolojia inayoangazia sarufi zalishi. Katika mtazamo huu, uambishaji wa maneno uliangaziwa na jinsi uundaji huo hutawaliwa na vizuizi mbalimbali na sheria za fonolojia. Uwasilishaji wa data ulikuwa kupitia kwa maelezo ya kina, michoro na jedwali. Uchunguzi huu ulidhamiria kuchangia usomi wa Kiswahili kwa kuweka wazi athari za Sheng’ katika ukuaji wa lugha ya Kiswahili kimsamiati. Kadhalika, utafiti huu utawasaidia wanafunzi kuweka mipaka bayana kati ya msimbo wa Sheng’ na lugha ya Kiswahili sanifu

Visit

doi.org

Languages

KwaSwahiliSwahili, CoastalSwahili, Congo

Licenses

http://creativecommons.org/licenses/by/4.0

Similar

Kubainisha Kanuni na Sheria Zinazotawala Muundo wa Maneno katika Sentensi Sahili ya Ekegusii.Ulinganishi Wa Uundaji Wa Maneno Ya Kiswahili Na Ya KiarabuMakosa ya Kifonolojia Miongoni mwa Wanafunzi wa Kiigembe katika Ujifunzaji wa KiswahiliUtabirifu wa Makosa ya Utenganishaji na Uunganishaji wa Maneno katika KiswahiliMchango wa Mashairi ya Kiganda katika Kuendeleza Muundo wa Ushairi wa Kiswahili Kupitia Ufunzaji na UjifunzajiMuundo wa Mazungumzo ya Uuzaji na Ununuzi wa Nguo za Mitumba katika Soko Mjinga Kaptembwo

Kubainisha Kanuni na Sheria Zinazotawala Muundo wa Maneno katika Sentensi Sahili ya Ekegusii.

Utafiti huu unalenga kubainisha kanuni na sheria zinazotawala muundo wa maneno katika sentensi sahil

Ulinganishi Wa Uundaji Wa Maneno Ya Kiswahili Na Ya Kiarabu

Makala hii imejadili suala la ulinganishi wa uundaji wa maneno ya Kiswahili na Kiarabu. Katika makal

Makosa ya Kifonolojia Miongoni mwa Wanafunzi wa Kiigembe katika Ujifunzaji wa Kiswahili

Makala haya yananuia kuainisha na kuchanganua makosa ya kifonolojia miongoni mwa wanafunzi wanaozung

Utabirifu wa Makosa ya Utenganishaji na Uunganishaji wa Maneno katika Kiswahili

Uandishi ni mchakato unaohitaji umakini ili kinachoandikwa kieleweke kwa msomaji kwa namna iliyokusu

Mchango wa Mashairi ya Kiganda katika Kuendeleza Muundo wa Ushairi wa Kiswahili Kupitia Ufunzaji na Ujifunzaji

Wanafunzi wengi nchini Uganda wanachukulia utanzu wa ushairi wa Kiswahili kuwa mgumu na wanapata ugu

Muundo wa Mazungumzo ya Uuzaji na Ununuzi wa Nguo za Mitumba katika Soko Mjinga Kaptembwo

Mazungumzo ndio njia mojawapo ya kuchochea maingiliano baina ya watu. Lugha ya mazungumzo hutokea ka