Logo Lanfrica
  • Home
  • Atlas
  • Insights
  • Docs
  • Sign in

© 2026 Lanfrica. All rights reserved. All copyrights of the resources shown on the Lanfrica website belong to the original copyright holders, unless explicitly stated otherwise.

Uhusika katika Vichwa vya Habari za Siasa

Domain:

natural language processing
Creator:
FidJacLeo
Publisher:
Eas
Host:
Uhusika ni dhana ya kisarufi ambayo hutumiwa kuonyesha dhima ya maneno katika tungo. Dhana hii ni muhimu katika uchambuzi wa tungo kwani hunuia kuwasilisha ujumbe wa kisemantiki uliogubikwa katika muundo wa ndani. Makala hii inadhihirisha dhana mbalimbali za uhusika na jinsi zinavyojitokeza katika vichwa vya habari za siasa zilizoko kwenye magazeti teule ya Taifa Leo. Nadharia ya uhusika iliyoasisiwa na Charles Fillmore mnamo mwaka wa 1968 imeongoza uchunguzi huu. Utafiti huu umefanywa baada ya kubaini kuwa wasomaji mbalimbali wa gazeti hufasiri maana anuwai kwenye kichwa kimoja cha habari za siasa. Jambo hili husababisha utata wa kimaana na uenezaji wa jumbe zisizo thabiti katika jamii, hivyo basi, kuzalisha migogoro ya kisiasa nchini. Upekuzi wa yaliyomo kwenye matoleo ya gazeti la Taifa Leo ambayo yametawaliwa na vichwa vya habari za siasa na kuchapishwa kati ya mwaka 2017-2019 ni msingi wa data ya utafiti huu. Vichwa vya habari za kisiasa kumi na nane vilisampulishwa kimakusudi na kutumika katika uchambuzi wa uchunguzi huu. Data katika makala hii imewasilishwa kupitia mfumo wa majedwali na maelezo. Matokeo ya utafiti huu yameshikilia kwamba, mahusiano kati ya kitenzi na nomino au kiwakilishi chake katika sentensi hubainisha aina ya uhusika. Uchunguzi huu una umuhimu kwa wasomi wa magazeti na taifa kijumla. Wasomaji wa magazeti wameongozwa na kigezo cha dhima ya maneno katika tungo ili kudondoa maana sahihi katika vichwa lengwa vya habari za kisiasa na kupitisha fasiri hiyo moja kwa wanajamii.

Visit

doi.org

Tasks

semantic role labelling

Languages

AmbaAnuakKunamaKwa

Licenses

http://creativecommons.org/licenses/by/4.0

Similar

Tofauti kati ya Majukumu na Maumbo ya Uhusika Katika Vichwa vya Habari za Siasa Kwenye Gazeti la Taifa Leo la Kenya.Udondoshaji wa Vipashio katika Vichwa vya Magazeti ya Kiswahili

Tofauti kati ya Majukumu na Maumbo ya Uhusika Katika Vichwa vya Habari za Siasa Kwenye Gazeti la Taifa Leo la Kenya.

Makala hii inaonyesha tofauti iliyopo kati ya majukumu na maumbo ya uhusika katika vichwa vya habari

Udondoshaji wa Vipashio katika Vichwa vya Magazeti ya Kiswahili

Uandishi wa magazeti umeonekana kuwa wa kipekee kwani hutumia mitindo mbalimbali ya uandishi ukiwamo