Logo Lanfrica
  • Accueil
  • Atlas
  • Analyses
  • Documentation
  • Sign in

© 2026 Lanfrica. Tous droits réservés. Tous les droits d'auteur des ressources affichées sur le site Web Lanfrica appartiennent aux détenteurs de droits d'auteur d'origine, sauf indication contraire explicite.

Dhima ya Methali Kinzani

Domaine:

natural language processing

Type de record:

paper
Créateur:
ChuJos
Éditeur:
Uni
Hôte:
Maadili katika jamii ni kipengele muhimu cha utamaduni na aghalabu huwasilishwa kupitia methali. Kimsingi, methali ni kauli za kifalsafa zinazotumiwa kuelezea na kuelekezea masuala kuhusu maisha ya wanajamii. Watu wanapozungumza, methali hujitokeza kama matini za ndani kwa ndani. Hivyo, methali hubeba ujumbe wa jumla unaohitaji kupatanishwa na miktadha ya kijamii. Mazingira haya huakisi mtazamo na tajiriba za jamii. Methali zinapotumiwa, huwa kurunzi ya kuukoleza zaidi ujumbe. Zinapotumika katika mazungumzo, matarajio ni kuibua jibu au tendo; kuonya kwa kuzingatia utamaduni wa jamii; kusuta matendo na kukemea matendo hasi ya watu. Katika uelekezaji wa maadili katika jamii, methali hutoa maelezo au kusuta kwa kuzingatia misimamo ‘mikali’. Methali hizo zimekuwa zikichukuliwa kwa ujumla kuwa zinapingana na zina mwelekeo hasi. Makala haya yanahakiki dhima ya methali kinzani katika kubainishia zaidi ujumbe wa kimaadili. Aidha, inabainishwa kuwa, methali zaidi ya moja zinaweza kutumiwa katika uwasilishaji wa ujumbe wa jumla na uelekezaji wa maadili katika jamii. Methali kinzani ni msingi katika kujengea mazingira ya uwajibikaji binafsi au wa kikundi cha watu.

Visit

doi.org

Languages

HayaKwa

Similaires

Mielekeo Ya Wanafunzi Wa Kidato Cha Tatu Na Cha Nne Kuhusu Methali Kinzani: Uchunguzi Katika Shule Za Upili Katika Kata Ya Township, Kaunti Ya Kitui; Kenya.“Wahenga walisema dalili ya mvua...” Uchunguzi wa Dhima za Viashiria vya Utendaji wa Methali katika Nyimbo za DansiDhima ya Vipengele vya Fani katika Uwasilishaji wa Ujumbe Unaorejelea Ugonjwa, Uuguzi na Tiba katika Methali teule za KiswahiliDhima ya Kialami Pragmatiki ‘Hivi’ katika Mawasiliano ya KiswahiliDHIMA YA VITABU VYA FASIHI TAFSIRIWA YA KIGENI KWA FASIHI YA KISWAHILIDhima Katika Mawasiliano ya Ushairi wa Jando Katika Jamii ya Watachoni, Kaunti ya Bungoma

Mielekeo Ya Wanafunzi Wa Kidato Cha Tatu Na Cha Nne Kuhusu Methali Kinzani: Uchunguzi Katika Shule Za Upili Katika Kata Ya Township, Kaunti Ya Kitui; Kenya.

Ukinzani ni dhana ambayo imefasiliwa kama ubishi au upinzani. Ukinzani katika methali za Kiswahili u

“Wahenga walisema dalili ya mvua...” Uchunguzi wa Dhima za Viashiria vya Utendaji wa Methali katika Nyimbo za Dansi

Methali ni utanzu unaotumiwa katika mawasiliano ya kawaida na katika utendaji wa tanzu mbalimbali z

Dhima ya Vipengele vya Fani katika Uwasilishaji wa Ujumbe Unaorejelea Ugonjwa, Uuguzi na Tiba katika Methali teule za Kiswahili

Maishani binadamu huathiriwa na magonjwa mbalimbali yasababishayo changamoto za kiafya, kijamii na k

Dhima ya Kialami Pragmatiki ‘Hivi’ katika Mawasiliano ya Kiswahili

Makala hii inahusu dhima za kialami pragmatiki hivi katika mawasiliano ya Kiswahili. Data za makala

DHIMA YA VITABU VYA FASIHI TAFSIRIWA YA KIGENI KWA FASIHI YA KISWAHILI

Before independence there was a dearth of publications in Kiswahili literature. Due to that scarcity

Dhima Katika Mawasiliano ya Ushairi wa Jando Katika Jamii ya Watachoni, Kaunti ya Bungoma

Makala haya yalilenga kuchunguza dhima ya mawasiliano ya ushairi wa jando kwenye jamii ya Watachoni