This repository supports participatory co-creation of an AI SMS prototype using low-power AI and feature phones to generate short message texts for advancing environmental justice among the Ogiek people in Mau Forest, Kenya. It also includes tools and resources that can be customized for non-extractive, participatory research and ethical co-design
# Muhtasari wa Mradi
Mradi huu wa ujumbe mfupi wa akili bandia, ulifadhiliwa na Mozilla Technology Fund, na unaongozwa na Lusike Mukhongo, Chad Edwards, Autumn Edwards, na Cynthia Klekar-Cunningham,kwa msaada wa Cody Thornell na Khang Nguyen. Lengo la mradi ni kutengeneza mfano wa mfumo wa ujumbe wa SMS unaoendeshwa na teknolojia ya AI kwa ajili ya jamii ya WaOgiek wanaoishi katika Msitu wa Mau. Kupitia mfumo huu, wanajamii wataweza kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kwa nambari maalum na kupokea majibu kutoka kwa chatbot kuhusu historia ya WaOgiek, uhifadhi wa misitu, maamuzi ya kisheria, na mengineyo. Mradi huu umechagua kutumia simu za kawaida, pia zinajulikana kama kabambe, kwa sababu hazihitaji intaneti, zina betri zinazodumu kwa muda mrefu, na ni nafuu – hivyo kuziwezesha kuwa rahisi kupatikana na jamii zilizo na rasilimali chache.
Lengo kuu la mradi huu lilikuwa kubaini jinsi mfumo wa ujumbe wa maandishi ulioboreshwa kwa teknolojia ya AI pamoja na tovuti vinaweza kusaidia kwa ufanisi watu wa jamii ya WaOgiek katika juhudi zao za kutetea usalama wa chakula, haki za ardhi, na utunzaji wa Msitu wa Mau kupitia kubadilishana taarifa, kuratibu matukio ya kijamii, na kuhifadhi maarifa ya asili ya WaOgiek.
Tulipata maarifa ya data kutoka kwa mahojiano, Majadiliano ya Vikundi Tarajiwa (FGDs), uchunguzi wa kietnografia wa juhudi za upandaji miti upya katika Msitu wa Mau, na warsha ya pamoja ya ubunifu na majaribio ya matumizi.
Ili kukamilisha mfumo wa SMS, tulishirikiana na jamii kuunda tovuti (sautiyaogiek.com) kama jukwaa la kidijitali linalobadilika kwa ajili ya kuhifadhi na kushiriki hadithi, sauti, na historia za mdomo za jamii ya WaOgiek. Tovuti hii ni hazina hai ambapo maarifa ya jamii yanaweza kurekodiwa, kufikiwa, na kusherehekewa. Kwa kutoa kitovu kimoja cha taarifa za kihistoria, maonyesho ya kitamaduni, rasilimali za kisheria, na juhudi za kimazingira, tovuti hii inakuza ujifunzaji kati ya vizazi na kuimarisha kumbukumbu ya pamoja ya jamii. Pia inaongeza …