Tunaona mbali, takwimu ndo darubini na tutafika tuendako kwa ushirikiano
# mboni_ya_takwimu
Taasisi mbalimbali hutoa takwimu kwa mambo mbalimbali juu ya jamii, uchumi na utamaduni wa nchi yetu.
Lengo kuu la mradi huu ni kuwezesha jamii ya watanzania kuweza kuelewa kwa urahisi takwimu hizi.
Tunaamini kwa kuhusianisha takwimu zilizopita na takwimu mpya wananchi wanaweza kuelewa kwa urahisi zaidi tunapotoka, tulipo na tunapokwenda.
Tunatarajia kuwa kupitia mradi huu tunaweza tengeneza programu tumishi ambayo itawezesha.
1. Kukusanya takwimu kutoka taasisi mbalimbali na kuzihifadhi pamoja
2. Watumiaji kuweza kuona na kuhusianisha takwimu kwa (timeline) wakati tofauti.
3. Watumiaji kuweza kuchagua seti ya takwimu wanazohitaji kutoka kwenye seti kuu na kupata muonekano wa picha.
4. Watumiaji kuweza kusambaza (share) muonekano wa picha kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamii.
5. Watumiaji kuweza kujadili juu ya takwimu kupitia mitandao yao ya kijamii iliyoungwa na programu tumizi hii.
Mradi huu tutaufanya kwa njia ya programu tumishi ya wazi(open source program). Kwa njia hii mtu yeyote anaweza kuchangia kutengeneza programu hii.
Walengwa hasa wakiwa wanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma. Wanafunzi watapata fursa ya kujifunza kutengeneza programu tumishi kwa ushirikiano kupitia GitHub.
Haya ni mawazo ya mwanzo kabisa, njoo tujumuike kuamua nini kifanyike na tukifanye kwa pamoja.