Logo Lanfrica

Muundo wa Motifu ya Safari katika Riwaya za: Mzingile, Walenisi na Siku Njema

Domaine:

natural language processing

Type de record:

paper
Créateur:
SilOneAll
Éditeur:
Eas
Hôte:
Dhana motifu imevutia makini ya watafiti mbalimbali kote ulimwenguni. Ina maana kuwa dhana ya motifu ya safari ina mwauo mpana wa maandishi. Tafiti za Kitaifa na kimataifa na ambazo sampuli yake ziliwasilishwa kwa lugha mbalimbali kama vile Kiingereza, kumaanisha kwamba dhana motifu ya safari inachangamsha watafiti wengi. Makala hii inahusu muundo wa motifu ya safari katika riwaya za Mzingile, Walenisi na Siku Njema. Nadharia iliyoangazia makala hii ni nadharia ya mwingilianomatini. Kwa mujibu wa nadharia hii ni kuwa msomaji wa kazi ya sanaa anayesoma kazi za wasanii wengine kuihusu kama kazi aliyoisoma mara kwa mara, anakuwa msomaji maalumu. Makala hii ilitumia muundo wa kimaelezo katika ukusanyaji, uchambuzi wa data pamoja na uwasilishaji wa matokeo. Sampuli ya makala hii iliteuliwa kimakusudi. Sampuli hii ni riwaya za Walenisi, Mizingile na Siku Njema. Makala hii inafaa taaluma ya fasihi kwa kubainisha namna motifu ya safari hutumiwa na waandishi mbalimbali kukuza dhamira kuu

Languages

Similaires