Logo Lanfrica

Uhulutishaji katika Lahaja za Kiswahili: Mifano Kutoka katika Kitenzi cha Kipemba

Domaine:

natural language processing

Type de record:

paper
Créateur:
Oma
Éditeur:
Eas
Hôte:
Mofolojia ya kitenzi cha Kipemba ina uhulutishaji wa kiasi kikubwa. Uhulutishaji huo, huenda unaleta athari mbalimbali katika ismu na matumizi ya Kipemba. Hata hivyo, uhulutishaji huo haujachunguzwa na kuwekwa wazi athari zake. Makala hii imechunguza uhulutishaji na athari zake katika mofolojia ya Kipemba. Data zimekusanywa kwa mbinu ya dodoso, ambapo jumla ya watafitiwa 30 walioteuliwa kwa mbinu ya usampulishaji lengwa walitumika. Nadharia ya Kiunzi Rasmi cha Fonolojia Zalishi ilitumika katika uchanganuzi wa data uliofanywa kitaamuli. Data zilichanganuliwa kitaamuli na kuwasilishwa kwa njia ya majaduweli na maelezo. Matokeo yamedhihirisha kwamba kuna uhulutishaji wa namna mbalimbali unaopelekea kuundwa kwa vitenzi vipya vya Kipemba na hautokei kiholela, bali unafuata kanuni maalumu. Miongoni mwa uhulutishaji huo ni ule wa kitenzi kisaidizi, kitenzi kkuu, na kiulizi, uhulutishaji wa kitenzi na kielezi, uhulutishaji wa kitenzi kisaidizi na kitenzi kikuu, uhulutishaji wa kitenzi na kiulizi, na uhulutishaji wa kitenzi na shamirisho. Aidha, uhulutishaji katika kitenzi cha Kipemba una athari mbalimbali zikiwemo kuunda vitenzi vipya, kuongezeka kwa viambishi viangami katika Kipemba, kunapelekea kuongezeka kwa darajia za mofu katika ruwaza ya kitenzi cha Kipemba, kupelekea Kipemba kuonekana kuwa na udondoshaji mkubwa katika tungo zake, kupelekea tungo za Kipemba kuwa na maneno machache kuliko zile za Kiswahili Sanifu, kupekelea Kipemba kuwa kigumu kuliko Kiswahili Sanifu, na kudhihirisha upekee wa mofolojia, mofofonolojia, na mofosintaksia ya Kipemba. Makala hii ni muhimu katika taaluma ya lahajia na kuonesha upekee wa mofolojia ya kitenzi cha Kipemba. Kwa hivi, inapendekezwa uchunguzi wa uhulutishaji katika nomino za Kipemba na lahaja nyengine za Kiswahili.

Similaires