Logo Lanfrica

Usawiri wa Wahusika wa Kike katika Tamthilia za Sudana na Dunia Hadaa

Domaine:

natural language processing

Type de record:

paper
Créateur:
Joh
Éditeur:
Eas
Hôte:
Suala la mahusiano ya wanawake na wanaume ulimwenguni limekuwa na linaendelea kuwafikirisha wahakiki na wanafasihi kote duniani kwa karne nyingi. Katika kuikabili kadhia hii, kumeibuliwa nadharia na mitazamo mbalimbali inayojaribu kueleza namna ya kuleta maridhiano ili kutuliza mgogoro baridi usiosita kwa kusudi la kutafuta usawa wa kijinsia. Inabainishwa kuwa waandishi wa kike wanaendeleza usawiri huo hasi wa wahusika wanawake katika kazi zao. Inaelekea kuwa waandishi wa kiume huwasawiri wahusika wa kike kwa namna tofauti wakilinganishwa na waandishi wa kike. Ikiwa kauli hiyo ina mashiko, basi itakuwa sawa kudai kuwa waandishi wa kiume ndio wa kulaumiwa kwa kuendeleza usawiri hasi kwa wahusika wa kike. Pia, ni sawa kudai kuwa waandishi wanawake wanawasawiri wahusika wa kike kwa mtazamo chanya.  Lengo la makala hii ni kulinganisha usawiri wa wahusika wa kike katika tamthilia ya Sudana iliyoandikwa na Mazrui na Njogu (2006) na Dunia Hadaa ya Kisovi, (2007) ambazo zimeandikwa na waandishi wa jinsia tofauti. Makala hii inakisia kuwa pana uhusiano wa karibu baina ya jinsia ya mwandishi na usawiri wa mhusika wa kike. Pia, tunachukulia kuwa pindi mitazamo ya waandishi hawa itakapobainishwa itasaidia kukadiria uwezekano wa fasihi kuwa chombo madhubuti katika kufikia usawa wa kijnsia. Ili kufikia lengo hili, tumeongozwa na nadharia ya Ufeministi wa Baada-ukoloni. Nadharia hii imetuwezesha kutambua sifa za mwanamke mwafrika akisawiriwa na waandishi waafrika.

Similaires