Logo Lanfrica
  • Home
  • Atlas
  • Insights
  • Docs
  • Sign in

© 2026 Lanfrica. All rights reserved. All copyrights of the resources shown on the Lanfrica website belong to the original copyright holders, unless explicitly stated otherwise.

Mafumbo ya mwanamke katika mashairi teule ya Muyaka

Domain:

natural language processing
Creator:
She
Publisher:
Edi
Host:
Ikisiri Azma kuu ya makala hii ni kuchanganua mafumbo ya mwanamke wa Kiswahili wa karne ya kumi na tisa katika ushairi wa Kiswahili wa kipindi hicho. Kwa kutumia mashairi teule ya Muyaka, sura ya mwanamke huyo inabainishwa. Mwandishi anaongozwa na nadharia ya uhalisia hasa mhimili wa lugha unaosisitiza kuwa lugha sharti iambatane na wakati wake ili iweze kueleweka na wasemaji wake kimuktadha na kimatumizi. Mbali na kudurusu makala muhimu maktabani, mtafiti kwa kuelekezwa, alikwenda nyanjani kuwahoji Waswahili kuhusu utamaduni wao, hususan ule wa karne ya kumi na tisa. Katika makala hii, imedhihirika wazi kwamba, picha ya mwanamke wa Kiswahili inayochorwa katika mashairi teule ya Muyaka ina misingi yake katika utamaduni wa Waswahili wa karne hiyo. Makala hii itasaidia katika kuelewesha picha ya mwanamke wa Kiswahili wa karne ya kumi na tisa kama alivyosawiriwa katika ushairi wa Kiswahili wa karne hiyo.   Maneno muhimu: Mafumbo, uhalisia, utamaduni, shairi.   Abstract The main objective of this paper is to analyse puzzles depicting the Swahili woman of the 19th century as portrayed in the Kiswahili poetry of that era. Using Muyaka’s selected poems and employing the realism theory, this research identified several puzzles through the terminologies used, that contextualiSed and depicted the Swahili Woman of the 19th Century. The researcher used both library and field research. It is clear that the image of the Swahili woman as portrayed in the puzzles of the selected poems of Muyaka emanates from the Swahili culture of the 19th Century. This paper gives a clear understanding of the Swahili woman as portrayed in the Kiswahili poetry of the 19th Century.   Key terms: Puzzles, Realism, Culture, Poem.

Visit

doi.org

Languages

AmbaKwaMabaaleSwahiliSwahili, CoastalSwahili, CongoToposaUmbundu

Licenses

https://creativecommons.org/licenses/by-nc-sa/4.0

Similar

Uhalisia katika mashairi ya Kezilahabi (Dhifa)Taswira ya Mwanamke katika Kipindi cha Bi. Msafwari Runinga ya Citizen Nchini Kenya.Tamathali za Semi katika Mashairi ya Shaaban RobertMitazamo ya Ontolojia ya Waswahili katika Riwaya Teule za Muhammed Said AbdullaMifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za KiswahiliMitindo ya Uwasilishaji wa Suala la Afya Katika Matini Teule za Fasihi ya Kiswahili ya Watoto

Uhalisia katika mashairi ya Kezilahabi (Dhifa)

Ikisiri Fasihi ni kioo cha maisha. Humulika jinsi jamii ilivyo kwa kuangazia masuala mbalimbal

Taswira ya Mwanamke katika Kipindi cha Bi. Msafwari Runinga ya Citizen Nchini Kenya.

Utafiti huu unalenga kuchunguza na kutathmini taswira ya mwanamke katika kipindi cha Bi. Msafwari Ka

Tamathali za Semi katika Mashairi ya Shaaban Robert

Makala hii inachunguza Tamathali za Semi katika mashairi ya Shaaban Robert katika kazi zake za fasih

Mitazamo ya Ontolojia ya Waswahili katika Riwaya Teule za Muhammed Said Abdulla

Makala hii inafafanua namna mitazamo ya jamii ya Waswahili katika riwaya teule za Muhammed Said Abdu

Mifumo ya Kijamii katika Tamthilia Teule za Kiswahili

Mifumo ya kijamii inajitokeza waziwazi katika fasihi andishi ya Kiswahili. Mifumo hiyo huwakilisha m

Mitindo ya Uwasilishaji wa Suala la Afya Katika Matini Teule za Fasihi ya Kiswahili ya Watoto

Fasihi ya Kiswahili ya Watoto ni mojawapo ya tanzu za fasihi ya Kiswahili inayotumiwa na wasanii kuh