Makala hii inachunguza Tamathali za Semi katika mashairi ya
Shaaban Robert katika kazi zake za fasihi za Pambo la Lugha na
Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini.
Uchambuzi wetu ulijielekeza katika kuchunguza Uchambuzi wa
Kifafanuzi tamathali za semi zinazojitokeza katika mashairi ya
Shaaban Robert ndani ya vitabu teule na kwa kiasi gani msanii
aliitumia.
Katika makala hii tumegundua kuwa msanii alitumia tamathali za
semi kama mbinu ya kisanii kuwasilisha ujumbe kwa hadhira yake.
Sitiari. ,Tafsida, Takriri, Tashbiha, Tashhisi,
Tamathali za semi ambazo zimeonekana kutumiwa zaidi katika
mashairi hayo ni sitiari, tashibiha, tashihisi, tafsida na takriri.
Mwandishi pia alilenga kutumia Tamathali za Semi katika
katika ushairi wake ili kushughulikia baadhi ya masuala
ya kijamii, kama vile ukatili dhidi ya wanawake na nafasi
zao katika jamii.Hili ndilo lililofanya mashairi ya mwandishi kuwa na thamani ya kifasihi na kijamii, namtindo wake kuwa na mvuto katika jamii. makundi mbalimbali ya jamii ya Watanzania.