Logo Lanfrica

Mikakati ya Udumishaji wa Lugha ya Kishona Nchini Kenya

Domaine:

natural language processing

Type de record:

paper
Créateur:
MerBonSte
Éditeur:
Eas
Hôte:
Makala haya yanalenga kuchunguza mikakati mbalimbali inayotumiwa na Washona katika kudumisha lugha ya Kishona nchini Kenya. Washona ni Wabantu ambao asili yao ni nchi ya Zimbabwe na walifika nchini Kenya kuanzia mwaka wa 1959 kwa lengo la kuhubiri injili kupitia kwa dhehebu la Gospel of God. Washona wametagusana na jamiilugha mbalimbali nchini Kenya hasa katika kaunti ya Kiambu iliyo na hali ya wingilugha hasa kwenye mitaa ya Kinoo, Kikuyu, Kiambaa, Gitaru, na Githurai ambayo ni makazi ya Washona wengi wanaoishi nchini Kenya. Mtagusano wa lugha mbalimbali waweza kuhatarisha uthabiti wa kiisimujamii wa lugha ambayo ina idadi ndogo ya wazungumzaji na ambayo haina usaidizi kutoka asasi mbalimbali za kiserikali. Hali hii ndiyo inayoikabili jamiilugha ya Washona nchini Kenya. Makala haya yaliongozwa na nadharia ya uzalishaji kijamii ya Bourdieu (1977) ambayo iliendelezwa na O’Riagain (1994). Kupitia kwa mhimili wake wa kwanza unaosema kwamba kila kizazi hubuni na kuweka mikakati ya kurithisha kizazi kinachofuata utamaduni wake, nadharia hii inasisitiza mikakati ambayo jamiilugha huweka ili kudumisha lugha ambayo ni kipengele muhimu cha utamaduni. Utafiti huu ulifanyikia maktabani na nyanjani. Utafiti wa nyanjani ulifanyikia kwenye maeneo ambayo wanajamiilugha wa Kishona huishi ili kupata data iliyobainisha mikakati ambayo Washona wanatumia ili kudumisha lugha yao ya Kishona nchini Kenya. Jumuiya ya utafiti ilikuwa jamiilugha ya Washona wanaoishi katika mitaa mitano ya kaunti ya Kiambu. Sampuli ya utafiti huu iliteuliwa kimaksudi na kwa njia elekezi. Mbinu zilizotumiwa katika ukusanyaji wa data ni mahojiano, uchunzaji na mijadala ya vikundi vidogovidogo. Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa kutumia mbinu changamano. Matokeo yaliwasilishwa kwa njia ya maelezo na kuongozwa na nadharia ya uzalishaji kijamii. Kufuatia juhudi za UNESCO za kudumisha lugha asilia, utafiti huu ni wa manufaa kwa Washona wenyewe, taifa la Kenya na mataifa mengine kwa kuwa uliongezea data muhimu katika kuhifadhi lugha ya Kishona nchini Kenya

Similaires