Logo Lanfrica
  • Accueil
  • Atlas
  • Analyses
  • Documentation
  • Sign in

© 2026 Lanfrica. Tous droits réservés. Tous les droits d'auteur des ressources affichées sur le site Web Lanfrica appartiennent aux détenteurs de droits d'auteur d'origine, sauf indication contraire explicite.

Wakaa katika Hotuba Teule za Wanasiasa wa Kenya

Domaine:

natural language processing

Type de record:

paper
Créateur:
MukTit
Éditeur:
Eas
Hôte:
Makala hii inachunguza ubainishaji wa wakaa katika hotuba teule za wanasiasa wa Kenya. Baadhi ya wanasiasa hutoa hotuba zinazovuta makini ya wasikilizaji na wafuasi wao kwa mitindo tofauti. Mojawapo wa mbinu hii ya kimtindo ni usimulizi. Wakaa ni mojawapo wa kipengele cha kimtindo katika usimulizi. Tafiti kadha zimefanywa kubainisha wakaa na matumizi yake katika tanzu za fasihi andishi na fasihi simulizi (taz. Kwaka; 2015; Khamis; 2015; Muiya; 2018; Kinga; 2020; Asige, 2021). Licha ya hayo, tafiti hizi za awali hazikushughulikia wakaa kwa kuhusisha moja kwa moja si hotuba tu bali hotuba za kisiasa. Ni katika msingi huu ndipo makala hii imechunguza jinsi wakaa inavyojitokeza katika hotuba teule za wanasiasa wa Kenya. Makala hii imeelekezwa na nadharia ya Naratolojia iliyoasisiwa na mwanafalsafa Plato katika chapisho lake The Republic na baadaye ikaendelezwa na mwanafunzi wake Aristotle (1920) aliyewasilisha mawazo yake katika chapisho la The Poetics na wananaratolojia wa hivi majuzi Gennette (1980), Prince (1982) na Rimmon-Kenan (2002). Uchunguzi huu ulizingatia mawazo yake Rimmon-Kenan. Naratolojia ni stadi ya aina ya utendaji kazi wa usimulizi. Huangalia undani wa vifaa vinavyoongoza maelezo ya simulizi na ufahamu wa utendaji kazi wake. Data iliyotumika katika makala hii imetokana na kusoma machapisho maktabani kama vile tasnifu, majarida na vitabu. Halikadhalika, utazamaji, usikilizaji na uchambuzi wa hotuba teule za wanasiasa Mhes. Kenyatta, Odinga na Ruto katika mtandao wa YouTube ulihusishwa. Matokeo ya utafiti yamedhihirisha kuwepo kwa vipengele vya wakaa vya mpangilio, muda na idadi au umara katika hotuba za wanasiasa. Isitoshe, imebainika kuwa kipengele hiki cha usimulizi kimetumiwa kuendeleza maudhui, fani za lugha na kuchimuza wahusika

Visit

doi.org

Languages

KingaKwa

Licenses

http://creativecommons.org/licenses/by/4.0

Similaires

Upambanuzi wa changamoto za vijana kama inavyodhihirika katika riwaya teule za WaliboraUsawiri wa Wahusika wa Ajabuajabu katika Riwaya Teule za Kihalisiajabu za Shaaban Robert na za Euphrase KezilahabiMatumizi ya Usohalisia wa Kihistografia katika Nyimbo Teule za Kisasa za Injili za KikambaUsawiri wa mandhari kibibliotherapia katika hadithi fupi teule za kiswahiliUamilifu wa Ngazi ya Utambuzi katika Riwaya Teule za KiswahiliUchunguzi wa fani za lugha zilivyotumika kuibua changamoto za vijana katika riwaya teule za Kiswahili

Upambanuzi wa changamoto za vijana kama inavyodhihirika katika riwaya teule za Walibora

Utafiti huu ulilenga kubaini changamoto zilizowakabili vijana katika mazingira walimoishi kwa mujibu

Usawiri wa Wahusika wa Ajabuajabu katika Riwaya Teule za Kihalisiajabu za Shaaban Robert na za Euphrase Kezilahabi

Wahakiki na wataalamu mbalimbali wa kazi za fasihi wamejadili kwa mapana usawiri wa wahusika wa ajab

Matumizi ya Usohalisia wa Kihistografia katika Nyimbo Teule za Kisasa za Injili za Kikamba

Usohalisia ni kipengele muhimu kinachodhihirika katika tungo za kisasa za fasihi. Watunzi wa fasihi

Usawiri wa mandhari kibibliotherapia katika hadithi fupi teule za kiswahili

Mandhari huwa ni sehemu muhimu katika kazi ya Sanaa. Mtunzi hutumia mandhari kuibua maudhui na sifa

Uamilifu wa Ngazi ya Utambuzi katika Riwaya Teule za Kiswahili

Makala haya yanachunguza ngazi ya utambuzi na uamilifu wake katika riwaya za Kiswahili zilizoteuliwa

Uchunguzi wa fani za lugha zilivyotumika kuibua changamoto za vijana katika riwaya teule za Kiswahili

Utafiti huu ulilenga kuchunguza namna mbinu mbalimbali za lugha zilivyotumika kuibua na kudhihirisha