Logo Lanfrica

Maneno Muhimu : Chanzo cha lugha, Asili ya lugha, Nadharia za lugha , Lugha

Créateur:
Gac
Éditeur:
Zenodo
Hôte:avatar
Lugha ni mfumo wa sauti nasibu unaotumiwa na binadamu wenye tamaduni yao ili kuwasiliana. Je, lugha ilitoka wapi na ni nani iliyeiunda? Imekuwa ni kawaida ya watu kujaribu kuelewa kule lugha ilikotoka. Jambo hili limepelekea kuwepo kwa nadharia mbalimbali kadri wataalamu mbalimbali walijitokeza huku wakijaribu kufichua kilinge hiki cha lugha. Kwenye makala haya tumejaribu kuchunguza nadharia hizi mbalimbali na ambazo zimetusaidia kuelewa chanzo cha lugha ni kipi na ni akina nani waliokuwa wa mwanzo kuitumia. Vile vile, tumeweka ufafanuzi wa jinsi ilivyosambaa hadi kufikia kutumiwa na watu wengi. Pia, tumeonyesha mbona kuna lugha mbalimbali. Usomi wa maktabani ndio uliokuwa njia kuu ya kupata data yetu iliyoendeleza kazi hii. Kulikuwa na hatua nne kwenye utafiti huu; kwanza tulianza na kuandaa nyenzo zetu za utafiti, pili tuk abaini marejeleo tuliotumia, tatu, tukapanga muda wa utafiti na mwisho tukaingia kwenye usomi wake huku tukinakili yale muhimu. Data tuliokusanya ni ile yenye maelezo na idhibati kuhusu chanzo cha lugha. Data hii tuliigawanya mara nne kulingana na kule ilieleza lugha ilikotoka. Kuna zile zilieleza kuwa lugha ilitokana na Mungu, zilizoeleza kuwa ilianza tu yenyewe kutokana na wigo, zilizoeleza kuwa ilitokana na utangamano wa watu na mwisho zile zilieleza kuwa ilitoka na maumbile ya watu. Tulijaribu kuonyesha upungufu kwa kila nadharia na jinsi nadharia hizi zinavyokamilishana.Maneno Muhimu: Chanzo cha lugha, Asili ya lugha, Nadharia za lugha, Lugha

Similaires